Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
MKUTANO MKUU WA CCM KUFANYIKA JANUARI 18-19, 2025
MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unatarajia kufanyika Januari 18 hadi 19 mwaka huu ukiwa na ajenda tatu ikiwemo kuziba nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CCM katika ukumbi wa White House jijini Dodoma leo, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amesema mkutano mkuu huo utakuwa na ajenda tatu.
Alizitaja ajenda hizo hizo ni kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo Ndugu Abdulrahman Kinana,kupokea kazi za Chama kuanzia mwaka 2022 hadi 2025 pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Ameeleza kuwa taarifa hizo za utekelezaji ilani ni kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)
Kuhusu mchakato wa kumrithi Kinana, amesema mrithi wa nafasi hiyo anatarajiwa kupatikana baada ya kamati kuu kuwasilisha mapendekezo ya jina kwa halmashauri kuu kisha halmashauri kuu kuwasilisha jina hilo kwa wajumbe wa mkutano mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura.
"Kumekuwa na uvumi, unaona vichwa vya habari kwamba CCM patashika, wafuatao watajwa kurithi nafasi ya Kinana, nani kati ya hawa atachukua nafasi ya Kinana, wengine wanakwenda mbali kuandika wafuatao kuchukua nafasi ya Kinana. Kila mmoja anaandika navyotaka.
"Nataka kusema kwamba, nafasi ya Makamu Mwenyekiti haigombewi, unaposema kinyang'anyiro kinatoka wapi wakati nafasi haigombewi wala haijazwi fomu?," alieleza.
CPA Makala alisisitiza: "Tutampata makamu mwenyekiti baada ya mapendekezo ya kamati kuu na halmashauri kuu, kisha jina la atakayeziba nafasi hiyo litawasilishwa katika mkutano kuu na hapo ndipo zitapigwa kura ya ndiyo au hapana."
"Hatukuwa kimya, Chama kinaongozwa kwa katiba, kina utaratibu wake, hatuwezi kuongozwa kwa hisia za watu. Kwa sasa Kamati Kuu imeona ndiyo muda muafaka kujaza nafasi hiyo," alisema.
CPA Makalla aibainisha kuwa mkutano mkuu utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, vinavyotarajiwa kufanyika Januari 16 mwaka huu.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.