Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI

alternative

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameongoza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa kutembelea Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ili kukagua maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025.

Ukumbi huo, wenye uwezo wa kuchukua takriban watu 3,000, unakarabatiwa kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha mazingira bora kwa mkutano huo muhimu. Mkutano huu utakuwa na agenda kadhaa, ikiwemo kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), kufuatia kujiuzulu kwa Komredi Abdulrahman Kinana mwaka jana.

Balozi Nchimbi, akiwa ameambatana na Manaibu Katibu Mkuu wa CCM, John Mongella (Bara) na Dkt. Mohamed Said Dimwa (Zanzibar), pamoja na wajumbe wa Sekretarieti, alishuhudia kasi kubwa ya maandalizi hayo, huku akiwapongeza wahusika kwa jitihada zinazofanywa kuhakikisha kila kitu kinakuwa tayari kwa wakati.

Kwa mujibu wa Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, maandalizi ya mkutano huo yamefikia hatua nzuri. Alitangaza rasmi kuanza kwa maandalizi hayo jana, tarehe 7 Januari 2025, akibainisha kuwa mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi